Fursa ya Ufadhili
Fursa ya Ufadhili wa Masomo (VETA)
Je, unatamani kupata ujuzi wa kazi za mikono na kujiajiri au kuajiriwa kwa urahisi? Hii ndiyo nafasi yako! Nyansaho Foundation inatoa ufadhili wa masomo kwa vijana wenye nia ya kujifunza fani mbalimbali kupitia vyuo vya VETA.
Kozi Zinazo Tolewa
Plumbing (Ufundi wa Mabomba)
Electrical Installation (Umeme Majumbani na Viwandani)
Gardening (Bustani na Kilimo cha Kisasa)
AC Maintenance (Matengenezo ya Viyoyozi)
Faida za Ufadhili
Kulipiwa ada ya masomo
Mafunzo ya vitendo (hands-on training)
Kukuandaa kwa ujuzi kwaajili ya kujiajiri au kuajiriwa
Sifa za Mwombaji
Awe tayari kujifunza kwa bidii
Awe na nidhamu
Awe na umri unaokubalika (tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi)
Jinsi ya Kuomba
Jaza fomu ya usajili katika ukurasa huu
Au wasiliana nasi kupitia: info@nyansahofoundation.or.tz